• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Halmashauri ya Wilaya ya Geita

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
        • TASAF
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maji
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Elimu Msingi
        • Utamaduni
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • UKIMWI
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
    • Viwanda
    • Biashara
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Uvuvi
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe.Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Elimu,Afya na Maji
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Wahe.Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Sheria ndogo
    • Mpango mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi/kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha

Afya

Mkuu wa Idara: Dr. Modest Buchard 

Halmashauri ya wilaya ya Geita imedhamiria kutoa huduma bora za afya kujenga maisha bora kwa watu ili kuimarisha wanajamii kuwa na afya bora katika kuendeleza na kujenga uchumi imara unaohimili ushindani na kutoa maamuzi kwa misingi ya utawala bora ili kupunguza umasikini.

Vituo vya kutolea huduma za Afya na Umiliki wake;

Halmashauri ya wilaya ya Geita ina jumla ya vituo 48 vinavyotoa huduma za afya ikiwa ni Vtuo 5 vya afya na Zahanati 43.

Mchanganuo wa Vituo hivyo pamoja na umiliki wake ni kama ifuatavyo:-

Vituo vya afya 5 vinamilikiwa na Serikali. Zahanati 34 zinamilikiwa na Halmashauri,zahanati 3 zinamilikiwa na watu binafsi, zahanati 4 zinamilikiwa na Mashirika ya Umma na zahanati 2 zinamilikwa na Taasisi za Umama(Magereza na Hifadhi ya Rubondo).

Idadi ya watumishi kulingana na kada

SN
KADA
IDADI
1.
Daktari
7
2.
Katibu wa afya
3
3.
Famasia
1
4.
Daktari wasaidizi
4
5.
Daktari wa meno msaidizi
1
6.
Daktari wa macho msaidizi
1
7.
Mteknolojia meno
5
8.
Afiasa Tabibu
33
9.
Tabibu msaidizi
7
10.
Afisa Muuguzi
0
11.
Afisa Muuguzi Msaidizi
42
12.
Wauguzi
105
13.
Mteknologia Madawa
3
14.
Mteknolojia Maabara
3
15.
Mteknolojia Msaidizi Madawa
0
16.
Mteknolojia Msaidizi Maabara
19
17.
Mazoezi ya viungo
0
18.
Mteknolojia wa macho
0
19
Afisa usatawi wa jamii
3
20
Afisa afya mazingira
4
21
Afisa afya mazingira wasaidizi
18
22
Wasaidizi wa afya
3
23
Wahudumu wa afya
50
24
Afisa lishe
1

JUMLA
313


Mambo muhimu yanayozingatiwa katika utoaji wa huduma;

Idara ya afya inazingatia mambo makuu yafuatayo katika utoaji wa huduma kwa umma:-

Kuweka viwango vya huduma:

  • Idara imeweka wazi viwango vya huduma ambavyo watumiaji wataweza kutarajia, kufuatilia kutathmini utendaji na kupima matokeo.

Kuwa wazi na kutoa habari

  • Idara imeweka wazi na kuwasiliana kwa lugha fasaha, kuwasaidia watu wanaotumia huduma za afya, na kutoa taarifa kwa wateja kuhusu huduma, gharama na utendaji wetu kwa mwaka.

Ushauri na ushirikishwaji

  • Idara inashauriana na kushirikiana na watumiaji wa huduma za afya waliopo ikiwa ni pamoja na wafanyakazi/wahudumu wa afya katika kutumia maoni yao ili kuboresha huduma za afya.

Kuhimiza upatikanaji na kutangaza ubora wa huduma

  • Idara inadhamiria kufanya huduma za afya kupatikana na kufikika kwa urahisi na kuwapa wateja uchaguzi pale inapowezekana kwa yeyote anayezihitaji. Vilevile kuhimiza matumizi ya teknolojia kwa kadri rasilimali zitakavyoruhusu.

Usawa kwa wote

  • Idara inahudumia wateja bila upendeleo, kuheshimu usiri, heshima na hadhi, kuwa wanyenyekevu na kutoa huduma mahususi kwa wenye matatizo maalum.Kila mtumishi na mteja/mtumiaji huduma atawajibika ipasavyo katika utoaji/upokeaji huduma na kwa usawa bila upendeleo wa aina yoyote.Mazingira yoyote yanayoashiria vitendo vya rushwa katika utoaji wa huduma yatapingwa vikali na yatapigwa vita na kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria za nchi.

Ufuatiliaji na urekebishaji

  • Idara inajitahidi wakati wote kurekebisha huduma haraka na kwa wakati, kujifunza kutokana na malalamiko, kuweka utaratibu wa wazi wa kushughulikia malalamiko na mapitio yaliyo huru kila inapowezekana.

Matumizi bora ya rasilimali

  • Idara inatumia rasilimali zilizopo kutoa huduma zinazolingana na thamani ya fedha za bajeti ya Serikali iliyotengwa kwa mwaka, michango ya wabia na watumiaji.

Uvumbuzi na uboreshaji

  • Idara inaendelea kutafuta njia za kuboresha huduma na vitendea kazi kulingana na mazingira yetu.

Kushirikiana na watoa huduma wengine

  • Idara inaratibu na kutafsiri sera, miongozo na viwango kwa vituo vya huduma (Hospitali, vituo vya afya, zahanati, kliniki na maduka ya dawa) ili kuhakikisha utoaji wa huduma bora.Pia Idara inashirikiana na sekta nyingine, vitengo na mashirika yasiyo ya kiserikali na watoaji huduma wengine ili kusaidia kutoa huduma bora kwa watumiaji na kuwajibika katika mambo yafuatayo:-
  1. Afya ya uzazi na motto.
  2. Kukabiliana na majanga yanayohusiana na afya.
  3. Tiba asili na tiba mbadala.
  4. VVU/UKIMWI na kifua kikuu.
  5. Usawa wa kijinsia.
  6. Nguvu kazi kwa maendeleo ya Afya.
  7. Udhibiti wa maji taka na taka ngumu na usafi wa mazingira kwa ujumla.
  8. Udhibiti wa vyakula na dawa.
  9. Udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza.
  10. Huduma kwa wagonjwa wa nje na wanaolazwa.
  11. Kukusanya taarifa/ takwimu sahihi zinazohusu afya kinga na tiba kwa wakati.

Majukumu mengine muhimu;

Dharura na Majanga

  • Maandalizi ya kukusanya rasilimali na nyenzo zinazohitajika kukabiliana namajanga zitafanyika kila mara kabla ya majanga (shughuli hii itakuwa endelevu).Kufuatilia na kutoa taarifa za majanga kwa mamlaka mbalimbali kama vile;Mkurugenzi Mtendaji (W), Mhe.Mkuu wa Wilaya na Katibu Tawala wa Mkoa

Ukaguzi wa Maduka ya Madawa, vituo vya tiba binafsi na maabara.

  • Ukaguzi unafanyika kupitia kamati za Chakula na Dawa za Kata na Halmashauri(W). Haitazidi miezi mitatu (3)/robo mwaka kwa Kamati ya Chakula na dawa yaHalmashauri ya Wilaya na Kamati za Kata kufanya Ukaguzi.

Ufuatiliaji wa leseni ya maeneo yanayotoa 

  • Huduma kwa Mama na Mtoto.Hii inafanyika ndani ya miezi Mitatu (3) baada yakupokea maombi

Ukaguzi wa maeneo ya kuuzia vyakula

  • Hii inafanyika ndani ya miezi mitatu (3) yaani kila robo mwaka

Uchangiaji wa ada za masomo

  • Idara kuchangia sehemu ya ada za masomo kwa watumishi wa afyawanaojiendeleza kulingana na bajeti na upatikanaji wa fedha, ruhusa na uchangiajiwa ada utazingatia vigezo na taratibu zilizopo.

Mahitaji ya dharura wakati wa milipuko ya magonjwa

  • Kufuatilia mahitaji ya dharura wakati wa milipuko ya magonjwa ya kuambukizana majanga ya afya ya mazingira kwa mamlaka husika ndani ya siku 3.

Tangazo

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA IMETOA TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI May 24, 2022
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA INAKUTANGAZIA UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA MTAKUJA KATIKA MAMLAKA YA MJI MDOGO WA KATORO June 15, 2022
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA IMETOA TANGAZO LA KUWAITA KWENYE USAILI WATENDAJI WA VIJIJI NA MADEREVA June 27, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI GEITA DC July 08, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI YAWAKUMBUKA AKINA MAMA WALIOJIFUNGUA NA WAFUNGWA WANAWAKE

    March 07, 2023
  • BARAZA LA MADIWANI GEITA DC LAPITISHA BAJETI YA BILIONI 87.2 KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024

    January 24, 2023
  • GEITA DC YAWEKA KAMBI KATIKA KATA YA NYARUGUSU KUTOA MSAADA WA KISHERIA

    December 14, 2022
  • DC SHIMO ATAJA UMOJA NA MSHIKAMANO KUWA NGUZO KUU YA MAENDELEO TUNAPOSHEREHEKEA MIAKA 61 YA UHURU

    December 07, 2022
  • Tazama zote

video

DED. WANGA AWATAKIA MTIHANI MWEMA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA WANAOJIANDAA KUFANYA MITIHANI YA TAIFA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Asili ya jina Geita
  • Fursa ya viwanda
  • Fursa ya madini
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI, 2021
  • Vivutio vya Utalii
  • Miradi itakayotekelezwa
  • Miradi inayoendelea
  • Orodha ya wahe.Madiwani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Bofya Hapa Kutuma,Kupokea na Kufuatilia Malalamiko,Mapendekezo,Maulizo na Pongezi Halmashauri ya Wilya ya Geita
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Watumishi Portal
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS)
  • Ofisi ya Rais TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Sehemu

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Geita

    Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita

    Simu: +225 282520061

    Mobile:

    Barua pepe: info@geitadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali na Majibu yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa