Halmashauri ya wilaya ya Geita imejaliwa kuwa na fursa nyingi za uwekezaji ikiwemo biashara katika mji wake mkubwa wa Katoro. Mji huu unakadiriwa kuwa na wafanyabiashara 2,000 wenye leseni.
Mji wa katoro umezungukwa na miji midogomidogo inayojishughulisha na uchimbaji wa madini ya dhahabu,uvuvi,kilimo pamoja na ufugaji. Pia mji umeunganishwa na barabara kuu itokayo jiji la Mwanza kuelekea nchi za Rwanda,Burundi na Uganda.Kutokana na sifa hizi mji wa Katoro ni kati ya miji inayokuwa kwa kasi nchini na kuufanya kuwa senta kubwa ya kufanyia manunuzi makubwa(Shopping center) ya bidhaa mbalimbli katika mkoa wa Geita na mikoa jirani.
Pamoja na biashara ya bidhaa za madukani,Halmashauri imejaliwa kuwa na mazao ya chakula ambayo yamechukuwa nafasi kubwa katika biashara kama vile mpunga,nanasi pamoja na mhogo.Aidha kuna uvuvi mkubwa wa samaki(Sangara,Sato na Furu) katika mialo takribani 40 katika kata ya Nkome na Izumacheli ndani ya ziwa Victoria.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa