• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Halmashauri ya Wilaya ya Geita

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
        • TASAF
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maji
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Elimu Msingi
        • Utamaduni
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • UKIMWI
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
    • Viwanda
    • Biashara
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Uvuvi
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe.Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Elimu,Afya na Maji
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Wahe.Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Sheria ndogo
    • Mpango mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi/kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha

Usafi na Mazingira


Mkuu wa Idara: Bi Hellen Eustacy

Majukumu ya Msingi  ya Idara;

Hifadhi ya Mazingira

  • Kutenga maeneo ya Upandaji Miti, Majani, Maua, ukataji Miti na Upendezeshaji Mazingira na kusimamia Kampeni ya Taifa ya upandaji miti.
  • Kuhamasisha Jamii kupanda Miti, Majani na Maua, ili kupendezesha Miji na maeneo mbalimbali.
  • Kuandaa na kufuatilia utekelezaji wa Mipango ya Halmashauri ya usimamizi wa Mazingira kwa kuzingatia Mpango kazi wa Taifa wa Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira.
  • Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa Sheria ndogo na miongozo ya kulinda Mazingira ikiwa ni pamoja na bioanui, Ardhi, Mazingira ya Mito, Maziwa Bahari na Mabwawa,
  • Kubaini maeneo ya hatari yanayohitaji usimamizi maalumu na kumshauri Waziri mwenye dhamana ya Usimamizi wa Mazingira kuhusu njia bora zinazoweza kutumika.
  • Kuandaa Taarifa ya Hali ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
  • Kusimamia utunzaji wa vyanzo vya maji kwa Kudhibiti utekelezaji wa shughuli yoyote inayoweza kuleta athari katika maeneo ya mito, maziwa, Bahari na Mabwawa.
  • Kubaini Bioanui zilizopo katika Halmashauri na hali ya uharibifu na uhifadhi wake.
  • Kusimamia utekelezaji wa mipango ya matumizi bora ya Ardhi ya Halmashauri.
  • Kuandaa na kutekeleza mikakati, mipango na programu za Halmashauri kwa kuzingatia Mkakati wa matumizi Salama ya Teknolojia ya Kisasa (Biosafety).
  • Kuhamasisha matumizi ya teknolojia ya nishati mbadala pamoja na majiko banifu.
  • Kuandaa na kutekeleza miradi mbalimbali kuhusu Usimamizi wa Hifadhi ya Mazingira.
  • Kutoa mapendekezo na kufuatilia hatua za kukabiliana na uharibifu wa maeneo yaliyoathirika kutokana na shughuli za uchumi zisizo endelevu (kama uchimbaji madini, kilimo, ujenzi, ufugaji n.k);

Udhibitiwa uchafuzi wa Mazingira(Ardhi,Maji na Hewa)

  • Kuandaa na kutekeleza programu za kutoa elimu ya Mazingira kwa Jamii kuhusu njia bora za kudhibiti uchafuzi wa Mazingira na athari zake.
  • Kuweka miongozo ya kupunguza athari za uchafuzi wa hewa ya ndani ya makazi (in-door pollution) inayosababishwa na shughuli mbalimbali kama vile matumizi ya nishati ya kuni, vinyesi vya mifugo na uchomaji wa madini ya zebaki.
  • Kufatilia na kutathimini athari za uchafuzi wa Mazingira katika makazi, viwanda, migodi, ujenzi, biashara, kilimo na ufugaji.
  • Kuandaa na kusimamia miongozo ya kutenganisha maeneo ya makazi ya watu, ofisi na taasisi za elimu na shughuli za kiuchumi kama vile ujenzi wa viwanda, madampo ili kudhibiti athari kwa afya na Mazingira.

Tathmini ya Athari ya Mazingira

  • Kufuatilia utekelezaji wa tathmini ya athari ya Mazingira [TAM] kwa shughuli zinazotakiwa kufanyiwa.
  • Kufuatilia utekelezaji wa mpango na masharti ya TAM kwa kila shughuli/mradi uliofanyiwa tathmini hiyo au kukaguliwa.
  • Kushirikisha umma katika maamuzi yanayoweza kuathiri Mazingira na katika uandaaji wa sera, mikakati, mipango na kufanya utafiti/uchunguzi wa uharibifu au athari ya Mazingira unaosababishwa na shughuli za kiuchumi au kijamii na kutoa taarifa kwa Mkurugenzi mkuu NEMC.
  • Kufuatilia na kutoa ushauri kuhusu maeneo yaliyoathirika kutokana na shughuli za uchumi zisizoendelevu kama vile uchimbaji madini holela, uvuvi haramu, kilimo kisichokuwa endelevu, ujenzi holela, ufugaji wa kuhamahama usiozingatia uwezo wa marisho n.k.
  • Kusimamia/kuratibu utekelezaji wa kazi za kamati za Mazingira na kamati za kudumu za Halmashauri zinazoanzishwa na sheria ya usimamizi wa Mazingira ngazi ya Halmashauri hadi kitongoji/mtaa;
  • Kuandaa na kutekeleza mikakati, mipango na program za Halmashauri kwa kuzingatia mkakati wa kitaifa wa kuhimili na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Udhibiti wa Taka Ngumu

  • Kubuni mbinu za kupunguza taka na kusimamia utekelezaji wake ili kupunguza uchafuzi wa Mazingira.
  • Kufanya tafiti/uchunguzi ili kubaini aina za taka zinazozalishwa kutoka katika masoko, makazi, maeneo ya barabara na taasisi pia kubuni njia bora za kupunguza, kutenganisha, kuhifadhi na kutupa taka;
  • Kusimamia Usafi katika mifereji ya kukusanya maji ya mvua na kuhakikisha inafanya kazi muda wote.
  • Kuweka vyombo vya kuhifadhi taka katika maeneo yote ya umma.
  • Kuainisha na kutenga maeneo kwa ajili ya ujenzi wa dampo za kisasa.
  • Kutoa amri za kuzuia utupaji ovyo wa taka wa aina zote katika fukwe, maeneo ya wazi, mito na mifereji ya maji ya mvua.

Changamoto za Mazingira

  • Uharibifu wa Misitu ya asili (Deforestation / Forest degradation).
  • Uharibifu wa Mifumo ya ikologia ya Maji (River and Wetland Degradation).
  • Mifumo na Vyanzo.
  • Uharibifu wa Ardhi (Land Degradation).
  • Kupotea kwa Bionuai ( Loss of Biodiversity).
  • Uharibifu na Uchafuzi wa Mazingira.
  • Mabadiliko Tabianchi (Climate Change).

Shinikizo (Pressure) 

  • Kasi ya uharibifu wa Mazingira inasababishwa na utupaji wa taka ovyo, ukosefu wa madampo ya kisasa, Kilimo cha Kuhamahama, upanuzi wa mashamba, Matumizi makubwa ya nishati ya kuni na mkaa, mifugo mingi kupita kiasi, uchimbaji holela wa madini, ukataji miti kwa ajili ya kuni, mkaa, nguzo na mbao, ujenzi wa miundombinu ya barabara unaoambatana na ufyekaji miti na misitu ovyo, ni mashinikizo yanayosababisha uharibifu wa Mazingira.

Hatua zinazochukuliwa kukabiliana na uharibifu wa mazingira

Halmashauri ya Wilaya ya Geita imechukua na inaendelea na mikakati na mipango endelevu ifuatayo:-

  • Kuondoa watu waliovamia Misitu kwa ajili ya makazi na shughuli za kilimo,uchimbaji wa madini na ufugaji.
  • Kutoza faini kwa wavamizi wa Misitu.
  • Kuhamasisha upandaji miti, utunzaji misitu na ufugaji nyuki wa kisasa kwenye misitu kwa wadau 234 wenye mizinga zaidi ya 1590).
  • Kuhamasisha jamii na kutoa elimu juu ya kilimo cha kutumia makinga maji na matumizi ya mbolea ya asili.
  • Kuhamasisha jamii na kutoa elimu kwa jamii juu ya utunzaji wa mazingira; kusimamia utekelezaji wa sheria ya Misitu 2002 na Usimamizi wa sheria ya Mazingira 2004 na kanuni zake.
  • Kushirikisha wadau mbalimbali muhimu katika kusimamia utunzaji wa mazingira.
  • Kuandaa miongozo ya kuzuia uharibifu wa Misitu katika maeneo ya uwekezaji,
  • kuendelea na kampeni ya upandaji miti million 1.5 kila Mwaka na kuhifadhi Misitu ya asili.
  • Kuhakikisha kuwa miradi yote inafanyiwa EIA na kuandaa mpango wa usimamizi wa mazingira (EMP).
  • Kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara.
  • Kuhamasisha jamii na kuendelea kutoa elimu juu ya matumizi ya nishati mbadala, majiko banifu na vyanzo mbadala vya kipato rafiki wa mazingira (Ufugaji samaki,nyuki, kuku, kilimo cha matunda).
  • Kusimamia zoezi la Usafi wa Mazingira kwa kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi.

Tangazo

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA IMETOA TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI May 24, 2022
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA INAKUTANGAZIA UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA MTAKUJA KATIKA MAMLAKA YA MJI MDOGO WA KATORO June 15, 2022
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA IMETOA TANGAZO LA KUWAITA KWENYE USAILI WATENDAJI WA VIJIJI NA MADEREVA June 27, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI GEITA DC July 08, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI YAWAKUMBUKA AKINA MAMA WALIOJIFUNGUA NA WAFUNGWA WANAWAKE

    March 07, 2023
  • BARAZA LA MADIWANI GEITA DC LAPITISHA BAJETI YA BILIONI 87.2 KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024

    January 24, 2023
  • GEITA DC YAWEKA KAMBI KATIKA KATA YA NYARUGUSU KUTOA MSAADA WA KISHERIA

    December 14, 2022
  • DC SHIMO ATAJA UMOJA NA MSHIKAMANO KUWA NGUZO KUU YA MAENDELEO TUNAPOSHEREHEKEA MIAKA 61 YA UHURU

    December 07, 2022
  • Tazama zote

video

DED. WANGA AWATAKIA MTIHANI MWEMA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA WANAOJIANDAA KUFANYA MITIHANI YA TAIFA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Asili ya jina Geita
  • Fursa ya viwanda
  • Fursa ya madini
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI, 2021
  • Vivutio vya Utalii
  • Miradi itakayotekelezwa
  • Miradi inayoendelea
  • Orodha ya wahe.Madiwani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Bofya Hapa Kutuma,Kupokea na Kufuatilia Malalamiko,Mapendekezo,Maulizo na Pongezi Halmashauri ya Wilya ya Geita
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Watumishi Portal
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS)
  • Ofisi ya Rais TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Sehemu

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Geita

    Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita

    Simu: +225 282520061

    Mobile:

    Barua pepe: info@geitadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali na Majibu yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa