Halmashauri ya Wilaya ya Geita inaendelea na utekelezaji wa mkakati wa uanzishaji viwanda, mpaka sasa viwanda 15 vipya vimeanzishwa na wadau mbalimbali. Viwanda 59 vya uchenjuaji wa dhahabu, 1 kusindika nanasi, 3 kusindika alizeti na 412 vya kuchakata nafaka vipo vinaendelea kufanya kazi. Hatua mbalimbali zimeshachukuliwa ili kufikia malengo ya mkakati huu ikiwemo:- kutambua fursa za uwekezaji, maeneo yenye vipaumbele, na mikakati ya kuanzisha viwanda hivyo.
Halmashauri katika kutekeleza sera ya viwanda imeweza kuainisha maeneo ya uwekezaji kwa wawekezaji wa ndani na wa nje yaliyopo katika Halmashauri kwa kuzingatia fursa za uendelezaji katika viwanda kutokana na shughuli kubwa za kiuchumi ambazo ni:-
Maeneo ya kipaumbe ya kiuchumi yaliyo ainishwa kwa ajili ya uwekezaji ni pamoja na Kilimo cha miwa kwa ajili ya kiwanda cha sukari, kilimo cha nanasi, nafaka mbalimbali na alizeti pia Uchimbaji na uchenjuaji wa madini ya dhahabu. Hii ni kutokana na kuwa na ardhi yenye rutuba nzuri, maeneo ya kutoshwa kwa ajili ya kilimo, hali ya hewa nzuri na mvua za kutosha, maeneo yenye madini ya dhahabu.
Halmashauri imedhamiria kuendeleza na kuanzisha viwanda vipya katika maeneo yote yenye fursa za uwekezaji kwa lengo la kukuza uchumi katika kuelekea nchi ya kipato cha kati.
Maeneo yaliobainishwa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda
NA
|
FURSA |
RASLIMALI ZILIZOPO
|
MAHALI |
UKUBWA (EKARI) |
1.
|
KIWANDA CHA SUKARI
|
|
|
|
2.
|
KUSINDIKA NANASI
|
|
|
|
3.
|
KIWANDA CHA KUSINDIKA NAFAKA
|
|
|
|
4.
|
KIWANDA CHA UCHENJUAJI WA MADINI YA DHAHABU
|
|
|
|
5.
|
KIWANDA CHA KUSINDIKA NYAMA/MAZIWA
|
|
|
|
6.
|
KIWANDA CHA KUSINDIKA ALIZETI
|
|
|
|
7.
|
KIWANDA CHA KUCHAKATA MUHOGO
|
|
|
|
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa