Halmashauri ya wilaya ya Geita imejaliwa kuwa na madini ya dhahabu kwa wingi katika kata za Nyarugusu,Magenge,Lwamgasa na Kaseme. Maeneo haya yana leseni za wachimbaji wadogowadogo pamoja na wa kati. Pia shughuli ya uchenjuaji wa mchanga ambao umechujwa dhahabu kwa mara ya kwanza unafanyika katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri.
Taratibu pamoja na ushauri wa kuwekeza katika sekta ya madini zinapatikana katika ofisi ya Afisa madini mkazi iliyopo mjini Geita mtaa wa General Tyre.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa