Wajumbe wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania Mkoa wa Geita (ALAT) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mhe. Vicent Busiga leo Mei 10,2025 wamefanya ziara ya kukagua miradi katika Jimbo la Busanda Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Wakiwa katika Kata ya Ludete, ALAT Mkoa wa Geita wametembelea mradi wa Ujenzi wa miundombinu ya upanuzi wa Shule ya Sekondari Lutozo.
Ujenzi wa Mabweni na Madarasa katika shule hiyo utaiwezesha shule hiyo kutoa elimu ya Kidato cha tano na Sita. Mradi huo una thamani ya Shilingi Milioni 372 fedha kutoka mfuko wa SEQUIP.
Wajumbe wa ALAT Mkoa wa Geita wametembelea Mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Shule ya Sekondari Lutozo inayaotarajiwa kupokea wanafunzi wa Kidato cha Tano Julai 2025
Vilevile wajumbe hao wametembelea Mradi wa Ujenzi wa Jengo la wodi ya wanaume, wodi ya Wanawake, wodi ya watoto, jengo la kuhifadhia Maiti, uzio wa Hospitali, Nyumba ya Mtumishi na ujenzi wa jengo la wagonjwa wa dharura (EMD) katika Hospitali ya Wilaya Katoro iliyopo Kata ya Ludete mradi wenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.2.
Wakiwa katika Hospitali hiyo, Wajumbe wamempongeza Mkurugenzi Mtendaji Ndg Karia Rajab Magaro kwa usimamizi mzuri wa fedha za Miradi.
" Tuwape maua yao ofisi ya Mkurugenzi na Idara ya Afya kwa usimamizi mzuri wa mradi " Amesema Mjumbe wa Kamati hiyo Mhe Batholomeo Manunga ambeye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato.
Ujenzi wa Hospitali hiyo ni matokeo ya ahadi ya aliye kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tano Hayati Dkt John Pombe Joseph Magufuli aliposimama kuwasalimia wananchi wa Buseresere Mkoani Geita na kuahidi kutoa Kiasi cha Shilingi Bilioni 1.5.
Mradi wa Ujenzi wa Jengo la wodi ya wanaume, wodi ya Wanawake, wodi ya watoto, jengo la kuhifadhia Maiti Hospitali ya Wilaya-Katoro umetembelewa na Wajumbe wa ALAT Mkoa wa Geita ambapo wamepongeza hatua za Mradi huo na Kuitaka Halmashauri kukamilisha taratibu zote mapema ili Majengo hayo yaanze kutumika
Pamoja na mambo mengine wajumbe wa ALAT wamempongeza Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mhe, Dkt, Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha nyingi za miradi ya maendeleo.
Jumuiya hii ilianzishwa tarehe 13 Desemba, 1984 mara baada ya kurejeshwa kwa Mfumo wa Serikali za Mitaa kwa Sheria Na. 7 na 8 za mwaka 1982 ambapo hujumuisha Halmashauri zote za Wilaya na za Miji, Miji Midogo na Vijiji Tanzania Bara.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa