• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Halmashauri ya Wilaya ya Geita

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
        • TASAF
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maji
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Elimu Msingi
        • Utamaduni
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • UKIMWI
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
    • Viwanda
    • Biashara
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Uvuvi
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe.Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Elimu,Afya na Maji
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Wahe.Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Sheria ndogo
    • Mpango mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi/kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha

DC SHIMO AWANUNULIA KALAMU NA MADAFTARI WANUFAIKA WA TASAF ILI KUWAPA HAMASA YA KUJIFUNZA KUSOMA NA KUANDIKA

Posted on: April 7th, 2022

Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe.Wilson Shimo Aprili 5, 2022 amejitolea pesa kwa ajili ya kununua kalamu na madaftari kwa wanufaika wa TASAF katika kijiji cha Chigunga ili wahamasike kujifunza kusoma na kuandika.

Mhe.Shimo alifanya ziara katika vijiji vya Isima na Chigunga vilivyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita ili kukagua utekelezaji wa mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF na kuzungumza na wanufaika wa mpango huo.

Baada ya kuzungumza na wanufaika hao alibaini kuwa wengi wao hasa wazee hawajui kusoma na kuandika hivyo kuwahamasisha kujifunza stadi hizo ili wafahamu taarifa muhimu zinazowahusu wao wenyewe ikwemo kiasi cha fedha wanachotakiwa kukipata.

Mhe.Shimo amesisitiza kuwa elimu hiyo itawasaidia pia kuepuka mapunjo yoyote wanayoweza kuyapata kwa sasa bila ya wao kujua, kutoka kwa mawakala wa malipo au hata ndugu wanaowatuma kuwapokelea fedha hizo huku akiwataka kutoa taarifa pale wanapohisi kudhulumiwa.

Akiwa katika kijiji cha Chigunga ameshauri kutafuta mwalimu Mstaafu ambaye anaweza kutumia muda mfupi tu kwa kila siku kuwafundisha wanufaika wasiojua kusoma na kuandika huku akitoa fedha taslimu kwa ajili ya kununua kalamu na madaftari, sambamba na kumteua kiranja mkuu, kazi ikibaki kwao ya kutafuta mwalimu wa kuwafundisha.

kwa upande wake mratibu wa Mpango huo wa kunusuru kaya masikini TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita Gabriel Evarist, amesema kuwa katika ziara hiyo ya Mkuu wa Wilaya wamebaini baadhi ya changamoto katika taratibu za malipo ya mwezi wa kwanza na wa pili huku akiahidi kuzishughulikia haraka iwezekanavyo.

Katika taarifa zao kwa Mkuu wa Wilaya zilizowasilishwa na Victoria  Malima Nyakina na Benziless Mayengo Wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha hizo ambazo zimewasaidia katika shuguli za kilimo na ufugaji, biashara ndogo ndogo, kuboresha makazi na kuwasomesha watoto.

Kijiji cha Isima chenye vitongoji vinne kina walengwa 146 ambapo kwa kipindi cha Julai 2015 hadi Machi 2022 kimepokea jumla ya Tshs.180,436,480/= ambazo zimelipwa kwa walengwa, huku kijiji cha Chigunga chenye walengwa 122 ambacho kimeingia kwenye mpango Januari 2022, kimepokea jumla ya Tshs.15,970,000/= malipo ya awamu mbili.  


Tangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI. June 05, 2025
  • TANGAZO LA KAZI GEITA DC September 10, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA September 16, 2024
  • Geita Mamlaka za Wilaya na malmaka za miji GP DOM.pdf September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MHE. WASIRA: AJENDA YA SERIKALI NI KUSIMAMIA MAENDELEO YA WANANCHI.

    June 18, 2025
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA YAPATA HATI SAFI, MHE. FATMA APONGEZA USIMAMIZI WA FEDHA ZA UMMA.

    June 13, 2025
  • UFUATILIAJI WAHIMIZWA KWENYE USIMAMIZI WA MIRADI WILAYA YA GEITA

    June 12, 2025
  • MKURUGENZI ASISITIZA HATUA KUCHUKULIWA KUDHIBITI UTORO SHULENI.

    June 05, 2025
  • Tazama zote

video

DED. WANGA AWATAKIA MTIHANI MWEMA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA WANAOJIANDAA KUFANYA MITIHANI YA TAIFA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Asili ya jina Geita
  • Fursa ya viwanda
  • Fursa ya madini
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI, 2021
  • Vivutio vya Utalii
  • Miradi itakayotekelezwa
  • Miradi inayoendelea
  • Orodha ya wahe.Madiwani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Bofya Hapa Kutuma,Kupokea na Kufuatilia Malalamiko,Mapendekezo,Maulizo na Pongezi Halmashauri ya Wilya ya Geita
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Watumishi Portal
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS)
  • Ofisi ya Rais TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Sehemu

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Geita

    Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita

    Simu: +225 282520061

    Mobile:

    Barua pepe: info@geitadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali na Majibu yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa