• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Halmashauri ya Wilaya ya Geita

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
        • TASAF
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maji
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Elimu Msingi
        • Utamaduni
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • UKIMWI
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
    • Viwanda
    • Biashara
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Uvuvi
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe.Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Elimu,Afya na Maji
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Wahe.Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Sheria ndogo
    • Mpango mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi/kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha

GEITA DC YAENDELEA NA UJENZI WA SHULE MPYA 23, ZA SEKONDARI

Posted on: November 21st, 2022

Na. Michael Kashinde

Halmashauri ya Wilaya ya Geita inaendelea na utekelezaji wa ujenzi wa shule mpya za sekondari 23 kutoka kiasi cha bilioni 5 na milioni 340 (Tshs. 5,340,000,000/=) zilizotolewa na Serikali kuu kupitia TAMISEMI kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 267 vya madarasa katika shule 39 kwa ajili ya kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2023.

Halmashauri ya Wilaya ya Geita kupitia vikao vyake Maalumu vya Kamati za Maendeleo za Kata, Timu ya Menejimenti (CMT), Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango na Baraza la Madiwani, waliazimia kuanzisha shule mpya 23 za sekondari badala ya kujenga vyumba 267 vya madarasa katika shule 39 zilizopo kutokana na sababu mbalimbali.

Miongoni mwa sababu hizo ni pamoja na kuwa baadhi ya shule hizo tayari zina idadi kubwa ya wanafunzi ambapo yakiendelea kujengwa madarasa zaidi katika shule hizo, bado idadi ya wanafunzi itaendelea kuwa kubwa zaidi suala ambalo linaweza kuleta tena changamoto nyingine ya namna ya kuwaongoza au kuwasimamia wanafunzi hao.

Aidha wanafunzi wengi hutembea umbali mrefu wa kwenda na kurudi shuleni ambapo baadhi hutembea kilomita 20 na zaidi, hivyo kuanzisha shule mpya katika maeneo yao inaweza kuwa msaada kwa wanafunzi hao kwa kupunguziwa umbali wa kwenda na kurudi shuleni lakini pia kuna maeneo ya wazi yanayoruhusu kujenga shule mpya.

Sababu nyingine iliyoangaliwa ni utoro wa muda mrefu kwa wanafunzi unaosababisha pia matokeo hafifu ingawa chanzo kikubwa kikitajwa pia kuwa ni umbali wa kwenda na kurudi shuleni, hivyo kuanzisha shule mpya katika maeneo wanakotoka wanafunzi hao kunatarajiwa kupunguza utoro na kuongeza ufaulu na hamasa ya kusoma kwa wanfunzi wenyewe na jamii kwa ujumla.

Baadhi ya wananchi waliona changamoto hizo mapema na kuchukua hatua za  kuanzisha ujenzi wa shule mpya kwa nguvu zao ili kupunguza changamoto hizo, ambapo kwa sasa Halmashauri inaunga mkono juhudi zao kwa kuwapatia fedha za kukamilisha miradi hiyo.

Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Jemedari Samia Suluhu Hassan imeendelea kuonyesha kujali Sekta ya Elimu kwa kuboresha na kujenga miundombinu hiyo kwa gharama kubwa huku ikitazamia kuwasaidia watoto wa kitanzania kupata Elimu bora katika miundombinu bora pia, ambapo kupitia madarasa ya UVIKO 19  Halmashauri ya Wilaya ya Geita ilipata jumla ya vyumba 352 vya madarasa vinavyotumika kwa sasa kama ilivyokusudiwa.

Hivyo linabaki jukumu la kila mtanzania kujitafakari namna gani anauunga mkono juhudi hizo za Serikali katika kufanikisha hilo na ndio sababu kuu inayowafanya viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wanaendelea kuwahamasisha wananchi kushiriki katika miradi hiyo kwa kuchangia nguvu zao katika kuchimba msingi, kusogeza mawe, maji na vingine vinavyowezekana  kwa sababu ni hulka ya ustaarabu tu, ukifadhiliwa  nyama unatafuta chumvi.

 


Tangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO KWA VIKUNDI January 23, 2025
  • TANGAZO LA KAZI GEITA DC September 10, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA September 16, 2024
  • Geita Mamlaka za Wilaya na malmaka za miji GP DOM.pdf September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAHIMIZWA KULINDA AMANI NA UTULIVU KUELEKEA UCHAGUZI MKUU-CPA AMOS MAKALLA

    May 20, 2025
  • RUSHWA NI JANGA LINALOATHIRI MAENDELEO YA KIUCHUMI, KIJAMII NA KISIASA NCHINI-RAS GOMBATI.

    May 13, 2025
  • GEITA YAPATA MAJIMBO MAPYA YA UCHAGUZI.

    May 12, 2025
  • ALAT MKOA WA GEITA WAMPONGEZA MKURUGENZI GEITA DC USIMAMIZI MZURI WA MIRADI

    May 10, 2025
  • Tazama zote

video

DED. WANGA AWATAKIA MTIHANI MWEMA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA WANAOJIANDAA KUFANYA MITIHANI YA TAIFA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Asili ya jina Geita
  • Fursa ya viwanda
  • Fursa ya madini
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI, 2021
  • Vivutio vya Utalii
  • Miradi itakayotekelezwa
  • Miradi inayoendelea
  • Orodha ya wahe.Madiwani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Bofya Hapa Kutuma,Kupokea na Kufuatilia Malalamiko,Mapendekezo,Maulizo na Pongezi Halmashauri ya Wilya ya Geita
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Watumishi Portal
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS)
  • Ofisi ya Rais TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Sehemu

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Geita

    Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita

    Simu: +225 282520061

    Mobile:

    Barua pepe: info@geitadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali na Majibu yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa