MWENGE wa Uhuru 2024 unatarajiwa kupokelewa Mkoa wa Geita Septemba 30, 2024 na kukimbizwa katika Halmashauri 6 za Mkoa wa Geita ambazo ni Chato ( Septemba 30,) Bukombe (Octoba 1) Mbogwe (Octoba 2) Nyang’hwale (Octoba 3)Geita mji (Octoba 4) na Geita Dc (Octoba 5, 2024) huku ukibeba kauli mbiu isemayo “Tunza Mazingira na shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa ujenzi wa Taifa Endelevu.”
Katika kuendelea na maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ifikapo Octoba 5, 2024, Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani Geita ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Hashim Abdallah Komba Septemba 9 ,2024 imefanya ziara ya kukagua njia ya Mwenge wa Uhuru ili kuendelea kutoa hamasa kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika mbio za Mwenge wa Uhuru ambao utapokelewa katika viwanja vya shule ya msingi Bugulula ukitokea Halmashauri ya Mji wa Geita.
Wananchi wakiwa katika eneo la mapokezi ya Mwenge wa Uhuru katika viwanja vya shule ya msingi Bugulula wakati Kamati ya Ulinzi na Usalama ilipofanya ziara ya kukagua njia ya Mwenge wa Uhuru 2024
Kamati hiyo imetembelea miradi yote itakayotembelewa na Mwenge wa Uhuru ambapo imeendelea kutoa Hamasa kwa wananchi wa maeneo yote kujitokeza kwa wingi kuulaki Mwenge wa Uhuru ambao utazindua na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Geita ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Hashim Abdallah Komba ikiwa katika ukaguzi wa Njia ya Mwenge wa Uhuru unaotarajiwa kupokelewa Octoba 5, 2024 katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kupokelewa Octoba 5, 2024 kata ya Bugulula ambapo utakimbizwa sehemu mbalimbali ndani ya halmashauri na baadaye kukesha katika viwanja vya kituo cha mabasi kilichopo kata ya Nkome.
Wananchi wakiwa katika Kituo cha Afya Nkome wakati kamati ya Ulinzi na Usalama ilipotembelea miradi ya maendeleo itakayo zinduliwa na kufunguliwa na Mwenge wa Uhuru Octoba 5, 2024
Pamoja na hamasa iliyotolewa kwa wananchi kushiriki katika mbio hizo, pia kamati ya ulinzi na usalama imetumia nafasi hiyo kuendelea kuwakumbusha wananchi kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.
Mbio za Mwenge wa Uhuru zinachochea na kuhamashisha tunu za taifa ambazo ni amani, uzalendo, umoja na mshikamano ndani ya Taifa na pia kuchochea shughuli za maendeleo.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa