Msimamizi wa Uchaguzi Serikali za Mitaa ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita ndg Karia Rajabu Magaro leo September 16,2024 ametangaza majina na mipaka ya Vijiji na vitongoji ili kuwafahamisha Wananchi majina ya maeneo na mipaka ambayo itahusika katika kujiandikisha na upigaji wa kura katika Uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.
Msimamizi wa uchaguzi ngazi ya Halmashauri Ndg. Karia Magaro akimkabidhi mwakilishi wa watendaji wa kata hati ya maeneo ya utawala wa uchaguzi wa serikali za Mitaa.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita ina majimbo mawili ya Uchaguzi ambayo ni Jimbo la Busanda lenye jumla ya Kata 22 na Tarafa 2 huku Jimbo la Geita likiwa na Jumla ya Kata 15, Tarafa 2.
Katika Kikao hicho kilichowakutanisha Watendaji wa Kata, wajumbe wa vyama vya siasa, wasimamizi wa Uchaguzi ngazi ya Halmashauri, Waheshimiwa Madiwani, Mwenyekiti wa Halmashauri, imeelezwa kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Geita ina jumla ya Tarafa 4, kata 37, Vijiji 145 na vitongoji 593.
Wajumbe wa vyama via siasa na wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya halmashauri na waheshimiwa madiwani wakiwa katika kikao cha kupokea tangazo la Maeneo ya utawala katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.
Pamoja na hayo Msimamizi wa Uchaguzi ndg Karia Rajabu Magaro amewataka watendaji hao kwa niaba ya Wananchi kubandika Tangazo hilo katika maeneo yote yanayohusika.
Msimamizi wa uchaguzi ngazi ya Halmashari Nag. Karia Magaro ( kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Charles Kazungu ( kulia) katika kikao cha kutanganza maeneo ya utawala wa uchaguzi wa Serikali za mitaa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Mhe Charles Kazungu ametoa rai kwa wajumbe hao kufanya kazi kama sheria, taratibu na kanuni za Uchaguzi zinavyoelekeza ili kutimiza wajibu kama tume ilivyo waamini Kutekeleza majukumu ya Uchaguzi.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa