Mbunge wa jimbo la Geita vijijini, ndugu Joseph Musukuma amekabidhi kontena la vifaa tiba mbalimbali kwa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ndugu Ali Kidwaka kwa ajili ya kuboresha huduma katika hospitali ya wilaya,Nzera.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika katika hospitali ya Nzera, Musukuma amevitaja baadhi ya vifaa kuwa ni vitanda 20 vya kisasa vinavyotumia umeme , meza 3 za kisasa za operesheni, ultrasound,pamoja na mashine ya kuwapa joto watoto waliozaliwa kabla ya kutimiza siku(incubator).
Amesema katika kuunga mkono juhudi za raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwenye uboreshaji huduma za afya, Musukuma aliomba vifaa hivyo kwa marafiki zake Nchini Sweeden ambavyo kwa kawaida vingenunuliwa taklibani shilingi bilioni 3.
“Tumepiga magoti tumeomba kwa marafiki zetu, hili ni kontena la 2, ni msaada tumepewa bure tulichogharamia ni nauli ambapo kontena kama hili ni kama milioni 30,lile la kwanza mkurugenzi alitusaidia namshukuru sana”, alisema Musukuma.
Hata hivyo alisema kuna kontena lingine linakuja kutoka Uingereza ambalo ni kwa ajili ya kina mama, lengo likiwa ni kuhakikisha hakuna mgonjwa atakayelala chini hospitalini hapo.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmasahuri ya wilaya Geita Ali Kidwaka amemshukuru ndugu Musukuma kwa kazi kubwa anazozifanya kama vile kuhakikisha majengo yanajengwa, kuleta magari ya kubeba wagonjwa, kontena 2 za vifaa tiba na mengine mengi.
Aidha,, ndugu Kidwaka amesema atahakikisha anatunza vifaa hivyo, pia amewataka wananchi kushirikiana kwenye ulinzi na utunzaji wa vifaa.
Nae mganga mfawidhi wa Hospitali ya Nzera, ndugu Kaitila Mulusuri amesema ujio wa vifaa hivyo, utasaidia sana katika kuboresha huduma kwenye hospitali hiyo kwani kwa siku wanahudumia wagonjwa takribani 70-120, lakini pia uwepo wa mashine inayosaidia watoto wanaozaliwa kabla ya siku kupata joto (incubator)itasaidia watoto hao waweze kukua vizuri.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa