• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Halmashauri ya Wilaya ya Geita

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
        • TASAF
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maji
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Elimu Msingi
        • Utamaduni
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • UKIMWI
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
    • Viwanda
    • Biashara
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Uvuvi
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe.Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Elimu,Afya na Maji
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Wahe.Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Sheria ndogo
    • Mpango mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi/kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha

MKURUGENZI HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA AWA MBOGO, ATOA MAAGIZO MAZITO KWA KAMATI ZA UJENZI, WAZABUNI NA MAFUNDI-MIRADI YA SHULE

Posted on: November 19th, 2023

Na: Hendrick Msangi

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Karia Rajabu Magaro ametoa maagizo mazito kwa kamati za ujenzi, wazabuni na mafundi wanaotekeleza miradi mbalimbali katika Halmashauri hiyo.

Magaro ametoa maagizo hayo kwa nyakati tofauti alipokuwa akikagua maendeleo ya miradi ya shule kwenye kata mbalimbali za Halmashauri hiyo zinazojengwa kwa fedha za SEQUIP.

Ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake kufanya ziara kwenye miradi hiyo, Magaro alibaini uzembe unaotokana na kutokuwa na uwazi katika utekelezaji wa miradi hiyo unaosababishwa na mafundi waliopewa kazi za ujenzi, kamati zinazosimamia miradi hiyo ambazo zimekuwa zikichelewesha kupeleka vifaa na kupelekea mafundi kukaa bila kufanya kazi, pamoja na wazabuni ambao wamepewa jukumu la kusambaza vifaa vya ujenzi kwenye miradi hiyo.

Mradi wa Shule ya Sekondari Nyakaduha kata ya Nyakaduha Wilayani Geita.  Shule itaanza kupokea wanafunzi 120 kidato cha kwanza ifikapo Januari 2024

Alisema kamwe hawezi kukubaliana na uzembe wowote ambao unakwamisha kasi ya ujenzi wa miradi hiyo ya shule ya Sekondari Nyakaduha na shule ya Sekondari iliyopo kata ya Ludete ambapo amesema serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi hiyo ili watoto wa kitanzania wapate elimu katika mazingira mazuri.

“Uzembe wowote unaosababishwa katika miradi hii sitaufimbia macho, watachukuliwa hatua wote wanaokwamisha kasi ya ukamilishwaji wa miradi, hatuwezi kwenda kwa kubembelezana tunafanya kwa faida ya watoto wetu, fedha zipo toka mwezi wa sita, natoa maagizo kwa kamati za ujenzi ifikapo Novemba 30 mkabidhi kazi kwani muda uliowekwa kukamilisha ujenzi umekwisha” alisema Magaro.

Aidha aliziagiza kamati za ujenzi, kutokuwalipa mafundi wote wanaosababisha hasara kwenye miradi hiyo na badala yake fedha hizo zitumike kufanya kazi nyingine za miradi hiyo.

Pamoja na hayo, Mkurugenzi huyo alikagua vifaa vya ujenzi yakiwemo matofali kuona ubora wake ili kuepuka athari ambazo zinaweza kujitokeza kwenye majengo na kuwaagiza wahandisi kutokupokea vifaa kutoka kwa wazabuni ambavyo vipo chini ya kiwango mpaka watakapothibitisha ubora wake kabla ya malipo kufanyika.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Karia Rajabu Magaro( aliyesimama) akikagua ubora wa matofali katika shule ya Sekondari iliyopo kata ya Ludete. Mradi wa Shule una thamani ya shilingi 584,280,029

Akiendelea kukagua miradi hiyo alizitaka kamati hizo kufanya kazi kwa kushirikiana na kwa uwazi ikiwa ni pamoja na kuwasimamia mafundi na sio kuwaacha kujipangia muda wa kufanya kazi jambo ambalo linachelewesha ukamilishwaji wa majengo ya shule hizo.

Mkurugenzi huyo aliwatembelea wazabuni wote waliopewa kazi za usambazaji wa vifaa kwenye miradi ya shule hizo ili kuona utekelezaji wao ikiwa ni pamoja na kujua changamoto ambazo zinazowafanya kutokupeleka vifaa kwa wakati katika miradi waliyopewa.

Ukaguzi Mradi wa Shule ya Sekondari kata ya Ludete Wilayani Geita.

Kwa upande wa mradi wa jengo la utawala ambalo ofisi za Halmashauri zimejengwa , Magaro aliagiza watu wa manunuzi na wahandisi  kuhakikisha kazi zote zilizobaki zinakamilishwa kwa haraka na mafundi wawepo eneo la kazi (site) ili mpango wa kuhamia katika jengo hilo  ukamilike kwa uharaka.

Halmashauri ya wilaya ya Geita inaendelea kuishukuru serikali inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kutoa fedha nyingi kwenye halmashauri hiyo kwa ajili ya kuwaletea wananchi maendeleo ili waendelee kuwa na Imani na serikali yao.

 

 

 

Tangazo

  • HIZI HAPA AJIRA ZA KUMWAGA GEITA DC July 15, 2025
  • TANGAZO LA KAZI GEITA DC September 10, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA September 16, 2024
  • Geita Mamlaka za Wilaya na malmaka za miji GP DOM.pdf September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WATENDAJI WASIMAMIWE KUHAKIKISHA AFUA ZA LISHE ZINATEKELEZWA - MHE. KOMBA

    July 12, 2025
  • HALMASHAURI ZATAKIWA KUONGEZA UBUNIFU KWENYE UKUSANYAJI WA MAPATO.

    July 12, 2025
  • VIKUNDI 111 VYANUFAIKA NA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI HALMASHAURI YA WILAYA, GEITA

    July 11, 2025
  • MHE. KOMBA ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI WA OFISI YA KATA, BUGULULA.

    July 05, 2025
  • Tazama zote

video

DED. WANGA AWATAKIA MTIHANI MWEMA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA WANAOJIANDAA KUFANYA MITIHANI YA TAIFA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Asili ya jina Geita
  • Fursa ya viwanda
  • Fursa ya madini
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI, 2021
  • Vivutio vya Utalii
  • Miradi itakayotekelezwa
  • Miradi inayoendelea
  • Orodha ya wahe.Madiwani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Bofya Hapa Kutuma,Kupokea na Kufuatilia Malalamiko,Mapendekezo,Maulizo na Pongezi Halmashauri ya Wilya ya Geita
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Watumishi Portal
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS)
  • Ofisi ya Rais TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Sehemu

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Geita

    Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita

    Simu: +225 282520061

    Mobile:

    Barua pepe: info@geitadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali na Majibu yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa