• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Halmashauri ya Wilaya ya Geita

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
        • TASAF
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maji
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Elimu Msingi
        • Utamaduni
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • UKIMWI
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
    • Viwanda
    • Biashara
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Uvuvi
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe.Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Elimu,Afya na Maji
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Wahe.Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Sheria ndogo
    • Mpango mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi/kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha

Shule za msingi na sekondari zasisitizwa kuwatumia ipasavyo wadhibiti ubora wa shule

Posted on: July 16th, 2019

Afisa elimu mkoa wa Geita Yesse Kanyuma amewasisitiza wakuu wa shule za msingi pamoja na sekondari kuanzisha na kutumia ipasavyo kamati  za udhibiti ubora ndani ya shule ili kuboresha elimu na kuwezesha shule kuendeshwa kwa kufuata  misingi, sheria na taratibu za elimu nchini.

Hayo ameyaeleza alipokuwa kwenye ziara ya kufuatilia ujenzi wa maboma ; mikakati ya ufundishaji na ujifunzaji kwa madarasa ya mitihani; kusoma, kuandika na kuhesabu( KKK); utawala na uendeshaji wa shule katika shule za kata zilizopo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita na mkoa kwa ujumla.

Akizungumza na wakuu wa shule, maafisa elimu kata, wenyeviti na wajumbe wa kamati za bodi za shule pamoja na walimu shule za msingi na sekondari za Kagu, Bugulula na Bugando, Kanyuma amesema kuwa wadhibiti ubora wakifanya kazi zao vizuri na kutumiwa ipasavyo katika kufanya tathimini mbalimbali , itasaidia katika maendeleo ya elimu shuleni.

Katika ziara hiyo aliambatana na maafisa elimu taaluma kutoka idara ya elimu mkoa, baadhi ya watumishi wa idara za elimu msingi na sekondari Halmashauri ya wilaya Geita wakiwemo wakuu wa idara hizo amezitaka idara zote za shule kuwa na mpango mkakati wa ufundishaji, kumaliza mada kwa wakati,

Mkuu huyo amesisitiza pia uwepo wa mitihani ya kujipima kwa wanafunzi, kuwa na vikao vya taaluma kujadili masuala ya ufundishaji na changamoto, motisha kwa walimu na wanafunzi wanaofanya vizuri, wanafunzi kuwa na vikao vyao lakini pia amepongeza baadhi ya shule kwa kukamilisha ujenzi wa maboma kabla ya tarehe iliyopangwa.

Mkuu wa idara ya elimu msingi Halmashauri ya Wilaya ya Geita Saidi Matiko amesema wameweka taratibu mbalimbali za kudhibiti utoro wa walimu pia amewataka walimu kuweka maazimio kila wanapokutana kwenye vikao vyao ili kurahisisha utekelezaji wa shughuli za shule.

Kwa upande wake afisa elimu Sekondari Richard Mwakihaba amewataka walimu kuwajibika ipasavyo katika  ufundishaji  wanafunzi ili kuboresha ufaulu pamoja na kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano katika uboreshaji elimu pia kutoa elimu bila malipo.

Tangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO KWA VIKUNDI January 23, 2025
  • TANGAZO LA KAZI GEITA DC September 10, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA September 16, 2024
  • Geita Mamlaka za Wilaya na malmaka za miji GP DOM.pdf September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAHIMIZWA KULINDA AMANI NA UTULIVU KUELEKEA UCHAGUZI MKUU-CPA AMOS MAKALLA

    May 20, 2025
  • RUSHWA NI JANGA LINALOATHIRI MAENDELEO YA KIUCHUMI, KIJAMII NA KISIASA NCHINI-RAS GOMBATI.

    May 13, 2025
  • GEITA YAPATA MAJIMBO MAPYA YA UCHAGUZI.

    May 12, 2025
  • ALAT MKOA WA GEITA WAMPONGEZA MKURUGENZI GEITA DC USIMAMIZI MZURI WA MIRADI

    May 10, 2025
  • Tazama zote

video

DED. WANGA AWATAKIA MTIHANI MWEMA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA WANAOJIANDAA KUFANYA MITIHANI YA TAIFA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Asili ya jina Geita
  • Fursa ya viwanda
  • Fursa ya madini
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI, 2021
  • Vivutio vya Utalii
  • Miradi itakayotekelezwa
  • Miradi inayoendelea
  • Orodha ya wahe.Madiwani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Bofya Hapa Kutuma,Kupokea na Kufuatilia Malalamiko,Mapendekezo,Maulizo na Pongezi Halmashauri ya Wilya ya Geita
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Watumishi Portal
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS)
  • Ofisi ya Rais TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Sehemu

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Geita

    Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita

    Simu: +225 282520061

    Mobile:

    Barua pepe: info@geitadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali na Majibu yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa