Mpango wa kunusuru kaya masikini (TASAF III) ambao unatekelezwa katika sehemu mbalimbali umekuwa na mafanikio makubwa ambapo walengwa sabini na nne (74) katika kijiji cha Nyambaya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita kata ya katoma wamenufaika.
Katika kuhakisha maendeleo ya Tanzania yanakuwa na kuimarisha uchumi wa kati kupitia viwanda ifikapo 2025, Miradi mikubwa ya kilimo imezidi kuwa na tija ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Miradi ya kilimo cha zao la Nanasi,Mahindi na Mpunga ni miongoni mwa miradi inayotekelezwa na walengwa wa Mpango wa TASAF III ndani ya Halmshauri ya Wilaya ya Geita,huku fedha hizo pia zikiwanufaisha katika Mifugo na kuendesha vikundi vya mikopo vinavyowapa asilimi kumi (10%) kila mwezi hali inayowaongezea tija katika maendeleo.
Akiwa katika ziara ya kikazi Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel amewapongeza walengwa hao kwa hatua ya kujikwamua na kuendeleza miradi inayoleta tija kwa taifa na amewaasa wataalamu mbalimbali kutoka katika halmshauri kuwapatia mbinu mbadala walengwa ili kuongeza ufanisi katika undeshaji wa miradi hiyo.
Mhandisi Gabriel aliembatana na Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Ndugu,January Bikuba na wajumbe wa mpango wa TASAF III Wilaya na Mkoa, amepokea salamu za pongezi kutoka kwa walengwa hao kwenda kwa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Dkt John Pombe Magufuli kwa namna wanavyotekeleza mpango huo.
Mpango huo ulianza Mwaka 2015 ambao hadi sasa ni awamu ya ishirini na mbili (22) na umekamilisha miaka minne (4) ya tathimini na kuongeza weledi kwa walengwa kwani wamejiunga katika mfuko wa bima ya Afya na kuwekeza hisa, hadi sasa wana jumla ya Shilingi Milioni moja na laki sita(Tsh.1,600,000) Kutokana na marejesho ya wanakikundi.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa