KITENGO CHA UCHAGUZI
Mkuu wa Kitengo
Januari Bikuba
Utangulizi:
Kitengo cha Uchaguzi ni miongoni mwa vitengo 6 vya Halmashauri ya Wilaya ya Geita vilivyoanzishwa kwa mujibu wa Muundo wa Halmashauri wa mwaka 2012.
Kitengo hiki kilianzishwa mahususi kwa ajli ya kusimamia na kuratibu shughuli zote za uchaguzi Mkuu na Chaguzi ndogo za Urais, ubunge na Udiwani kwa mujibu wa Sheria za Uchaguzi, Kanuni za Uchaguzi na Maelekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika ngazi ya Halmashauri. Pia kitengo hiki kinawajibika kusimamia na kuratibu shughuli za Uchaguzi Mkuu na Chaguzi ndogo za Serikali za Mitaa kwa Mujibu wa Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Kanuni za Uchaguzi na Maelekezo ya Wizara yenye dhamana ya Serikali za Mitaa.
Dira:
Dira ya Kitengo hiki ni Kuwa kitengo madhubuti kitakacho weza kuchangia katika kuleta maendeleo ya wananchi kwa kujenga Halmashauri inayozingatia Utawala bora uliojengwa katika misingi ya Uchaguzi Huru, wa Haki na wa Mara kwa mara (Free, Fair and Frequent elections) kufikia 2025 .
Dhima:
Dhima ya kitengo hiki ni kuhakikisha kuwa Sheria na Kanuni za Uchaguzi zinasimamiwa ipasavyo kwa lengo la kuwawezesha Wananchi wote wenye sifa katika Halmashauri kupata fursa ya kushiriki kikamilifu katika kuwachagua viongozi wao kupitia uchaguzi ulio huru na wa haki.
Majukumu ya Msingi:
i.Kusimamia na kuratibu zoezi la Mgawanyo wa Maeneo ya utawala (Vitongoji, Vijiji na Kata) katika mipaka ya Halmashauri
ii.Kusimamia na Kuratibu zoezi la kuandaa orodha ya Wapiga kura wenye sifa katika Halmashauri
iii.Kusimamia na kuratibu uteuzi wa wagombea wenye sifa na kampeni za Uchaguzi
iv.Kusimamia na kuratibu zoezi la upigaji kura
Mafanikio:
Toka kuanzishwa kwake kitengo hiki kimeweza kupata mafanikio makubwa katika utekelezaji wa shughuli za Uchaguzi. Mafanikio hayo ni Pamoja na:
i.Kusimamia kwa ufanisi Uchaguzi mdogo wa Diwani wa Kata ya Nzera wa mwaka 2012
ii.Kusimamia kwa ufanisi Uchaguzi Mkuu wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2014
iii.Kusimamia kwa ufanisi zoezi kuandaa Daftari la kudumu la Wapiga kura kwa kutumia Mfumo wa BVR mwaka 2015 ambapo wananchi wote wenye sifa katika Halmashauri waliandikishwa
iv.Kusimamia kwa ufanisi Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2015
v.Kusimamia kwa ufanisi Uchaguzi mdogo wa Diwani wa Kata ya Nkome wa mwaka 2017
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa