UTEKELEZAJI WA MPANGO WA Taifa wa KUDHIBITI UKIMWI WILAYA YA GEITA
Mratibu wa Muitikio wa Mapambano dhidi ya UKIMWI Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Patricea L.Nsinde
1.0 UTANGULIZI
Halmashauri ya wilaya Geita inaendelea kutekeleza kikamilifu shughuli za kupambana na UKIMWI,ikilenga kufikia sifuri 3 katika mapambano dhidi ya UKIMWI ambayo ni kuzuia maambukizi mapya,kuondoa Unyanyapaa na ubaguzi na kutokomeza vifo vitokanavyo na UKIMWI ifikapo June 2018. Shughuli mbalimbali ziliandaliwa
kwa kuzingatia maeneo makuu 3 ya mkakati wa III wa Taifa wa kudhibiti UKIMWI wa mwaka 2013/2014 hadi 2017/2018 ambayo yanalenga :-
•Huduma za kinga
•Mazingira wezeshi
•Kupunguza makali yatokanayo na UKIMWI
2.0 UKIMWI UNAVYOAMBUKIZWA
Kutokana na matokeo ya utafiti uliyofanywa na ofisi ya takwimu ya taifa mwaka 2012 inaonesha kwamba katika wilaya yetu Virusi vya UKIMWI vinaambukizwa kwa njia zifuatazo:-
•Kufanya ngono na mtu mwenye VVU bila kutumia kondomu.
•Kuchangia damu yenye virusi vya UKIMWI.
•Mama mjamzito kumwambukiza mtoto wake aliyetumboni ,wakati wa kujifungua au wakati wa kunyonyesha.
2:1 Maeneo hatarishi yanayochangia kuenea kwa virusi vya UKIMWI:
Katika wilaya yetu maeneo yenye msongamano wa watu kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii yanaonesha kuwa na kiwango kikubwa cha maambukizi ikilinganishwa na sehemu nyingine.
Maeneo hayo ni pamoja na:-
•Maeneo ya machimbo ya dhahabu.
•Maeneo ya uvuvi wa samaki kandokando ya ziwa Victoria.
•Vituo vya magari makubwa yanayopita wilayani Geita kwenda mikoa na nchi jirani zinazopakana na nchi yetu.
•Mikusanyiko mbalimbali ya watu hasa nyakati za usiku.
•Maeneo ya kazi za kiofisi.
2.2 Mila, desturi,tabia na mazingira yanayochochea maambukizi
Baadhi ya mila, desturi na mazingira ya jamii yanachochea maambukizi ambayo ni pamoja na:-
•Ulevi
•Kurithi wajane
•Ndoa za wake wengi
•Ndoa zakulazimishwa(wasichana kuolewa wakiwa na umri mdogo)
•Ngoma za mapacha,bukwilima,kutibiwa kwa waganga wa jadi.
•Mfumo dume
•Asilimia ndogo ya wanaume waliotahiliwa ambao ni asilimia (46%)
•Watumishi walio oana kuishi mbali na wenza wao.
•FEDHA ZILIZOPOKELEWA
•Katika Mwaka wafedha 2015/2016 Halmashauri ya Wilaya iliidhinishiwa bajeti ya Tshs 125,610,000 kuanzia Julai 2015 hadi Aprili 2016 hakuna fedha iliyopokelewa mwaka huo lakini ikapokelewa mwaka wa fedha 2016/2017 ambapo ndipo shughuli zinatekelezwa.Halmashauri iliendelea kukamilisha shughuli chache zilizobaki katika mwaka 2014/2015 ambazo fedha yake ilikuwa jumla ya Tshs 51,600,000/= ambayo ilitumika katika maeneo yafuatayo:-
•
3.0 SHUGHULI ZILIZOTEKELEZWA KATIKA KILA ENEO LA MKAKATI :
•Katika kipindi Julai 2015 hadi Aprili 2016 jumla ya shughuli 13 zimetekelezwa kwa kila eneo kama ifuatavyo:-
•3.1:ENEO LA HUDUMA ZA KINGA (Tshs 9,734,615 /=)
•i. Kusambaza katoni 164 za kondomu za kiume katika kata 28.
•ii. Kuandaa na kuelimisha jamii kwa njia ya sinema katika vijiji 4
•iii. Kuandaa na kufanya majadiliano na wanafunzi324 waelimishajirika wa shule 56 za msingi na 6 za sekondari.
• iv.Kuandaa na kutoa mafunzo kwa wasanii 60 vijana waelimishaji rika nje ya shule.
•3.2 ENEO LA MAZINGIRA WEZESHI (Tshs 20,867,351 /=)
•i. Kuandaa na kufanya mkutano wa siku 1na viongozi wa jamii 150 juu ya UKIMWI.
•ii.Kufanya ufuatiliaji shirikishi wa shughuli za kudhibiti UKIMWI katika kata 28 wilayani.
•iii.Kuwezesha usimamizi na ukaguzi wa matumizi ya fedha za kudhibiti UKIMWI katika kata 28.
•iv.Kuandaa mpango bajeti na taarifa za utekelezaji za robo 3 na kuwasilisha kwa wakati.
•3.3:ENEO LA KUPUNGUZA MAKALI YATOKANAYO NA UKIMWI
•Jumla ya Tshs (Tshs 20,000,000/=) zilitumika kutoa mtaji kwa vikundi 14 vya watu 400 wanaoishi na VVU wenye kipato duni wanaotumia dawa za ARVs waliyoanzisha miradi ya uzalishaji mali
5.0 MAFANIKIO:
Katika kipindi hiki mafanikio yaliyopatikana ni :-
•Baadhi ya makundi yaliyo katika mazingira magumu yamepata msaada wa kujikimu.
•Kumekuwa na ongezeko la uelewa kwa jamii kuhusu UKIMWI.
•Mahusiano mazuri kati ya wilaya na wadau mbalimbali ndani na nje ya wilaya.
•Unyanyapaa umepungua katika jamii.
•Jumla ya watoa huduma 31 kwa wagonjwa wa UKIMWI nyumbani wamejengewa uwezo na kukabidhiwa baiskeli 31na shirika la pamoja tuwalee chini ya Jimbo Katoliki Geita.
6.0 CHANGAMOTO
Katika kipindi hiki changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa shughuli za kupambana na UKIMWI ni pamoja:-
•Kutopata fedha za utekelezaji wa shughuli zilizopangwa kwa mwaka wa fedha 2015/2016 kutoka Hazina.
• Ongezeko la muingiliano wa watu kutoka sehemu mbalimbali wanaokuja kwa shughuli za kiuchumi kwenye maeneo ya machimbo,visiwani na kandokando ya ziwa.
•Uhaba wa vitendanishi kwa ajili ya upimaji walau kwa mama wajawazito.
•Uchache wa wauza kondomu hasa maeneo ya vijijini.
•Ongezeko la vichocheo vya maambukizi kutokana na teknolojia
•Ongezeko la watoto yatima na walio katika mazingira tete.
7.0 MKAKATI NA UTATUZI WA CHANGAMOTO
•Kuongeza jitihada ya kuelimisha jamii kupambana na UKIMWI.
•Kuimarisha uraghibishi na huduma ya tohara kwa wanaume.
•Kuimarisha ukusanyaji wa rasilimali na kusimamia matumizi bora kwa ajili ya mapambano dhidi ya UKIMWI
•Kuimarisha huduma ya ushauri nasaha na upimaji wa virusi vya UKIMWI kwa hiari.
•Kuelimisha na kurahisisha upatikanaji na usambazaji wa kondom kwa wenye kuzihitaji.
•Kuboresha mfumo wa kutoa ushauri na misaada kwa walioathirika na kuathiriwa na UKIMWI.
•Kumarisha mfumo wa kukusanya na kusambaza taarifa na takwimu muhimu zinazohusu UKIMWI.
•Kuimarisha ushirikiano na wadau na kufanya shughuli zote kwa pamoja.
•Kuongeza bajeti ya fedha zitokanazo na vyanzo vya ndani ili kuboresha huduma kwa walengwa.
MWISHO
Kila mmoja akitimiza wajibu wake Geita bila maambukizi mapya,unyanyapaa na vifo vitokanavyo na UKIMWI Inawezekana.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa